15 Aprili 2013 - 19:30
Tanzania kutuma jeshi lake Congo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeazimia kupeleka vikosi vya Jeshi lake JWTZ nchini Congo kwa minaajili ya kulinda amani

Tanzania imefikia uamuzi huo baada y akuombwa na Umoja wa mataifa ipeleke vikosi vyake kwa ajili y akusimamia amani katika Jamhuri ya kidemoklasia ya Congo,ambapo nchi hii ipo katika machafuko ya ndani yanayosababishwa na waasi, machafuko ambayo yamedumu kwa muda mrefu.  Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi amesema:wamekubaliana na Umoja wa mataifa  kwamba hadi kufikia mwezi ujao vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania vitakuwa vimekwisha wasili Congo